EXHIBITS

English

Mlalo

(4°34'34.54"S, 38°20'58.17"E, mwinuko, mita 1402)

Utangulizi

Bonde la Mlalo ni sehemu muhimu katika Milima yote ya Usambara. Kama Bumbuli na Gare, Mlalo ilikuwa kituo muhimu cha kutengeneza mvua. Kwa sababu hali ya hewa kwa ujumla ni kame zaidi kuliko maeneo ya kilimo kusini na mashariki, wakazi wa Mlalo waliongezea kilimo cha bustani cha milimani kwa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga na mahindi ambacho walilima kwenye Kitivo kando ya Mto Umba. Ingawa ni mifereji michache tu iliyosalia leo, wakulima wa Mlalo walikuwa watalam wa umwagiliaji. Watu wa Mlalo nao wanajua ulimwengu mzima. Hapo zamani, watu wa Mlalo hawakusita kuhama kwa muda katika miji ya pwani kama Pangani, Mombasa, na Tanga, na katika maeneo mengine mengi ya Afrika Mashariki.

DNO-0153_UsambaraSlides-017.jpg